![]() |
| Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg |
Facebook imeingia makubaliano ya kuinunua WhatsApp, kwa
dola bilioni 16, imefahamika.
Mkataba huo ndio mkubwa zaidi kuwahi kufanywa na Facebook
mpaka sasa na unakuja baada ya tetesi zilizozagaa mwishoni mwa mwaka 2012 na
mwanzoni mwa mwaka 2013 kwamba Facebook na Google walikuwa wakipigana vikumbo
kutaka kuimiliki huduma hiyo maarufu ya utumaji ujumbe.
"WhatsApp inaelekea kuwaunganisha watu bilioni 1.
Huduma inayofikia kiwango hicho ni huduma yenye thamani kubwa,” amesema
mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg, katika taarifa yake. "Ninamjua Jan
[Koum, mwanzilishi wa WhatsApp] kwa muda mrefu na nimefurahi sana kushirikiana
naye pamoja na timu yake ili kuzidi kuifungua na kuiunganisha dunia.”

0 comments:
Post a Comment