![]() |
| Ndege ya jeshi la Libya iliyoanguka leo nchini Tunisia na kuua watu wote waliokuwemo. |
Kwa uchache watu 11 wamepoteza maisha baada ya ndege
moja ya madaktari wa jeshi la Libya kuanguka kusini mwa mji mkuu wa Tunisia, Tunis, baada ya injini kushindwa kufanya kazi.
Kwa mujibu wa msemaji wa huduma za dharura wa Tunisia,
bwana Mongi El Kadhi, ndege hiyo ilikuwa na watu 11 ambapo watatu walikuwa
madaktari, wagonjwa wawili na wafanyakazi sita.
Ndege hiyo iliteketea kabisa na hakuna aliyenusurika
katika ajali hiyo.
Muda mfupi kabla ya ndege hiyo kutoweka katika udhibiti
wa rada, rubani aliwasiliana na uwanja wa ndege wa Tunis na kuwaambia kuwa
injini ilikuwa imeshindwa kufanya kazi.
Ndege hiyo iliangukia shambani katika kijiji cha Nianou lakini
iliweza kuzikwepa nyumba zote.
Huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo,
inaelezwa kuwa hiyo ni ndege ya pili ya kijeshi kuanguka ndani ya wiki mbili
katika eneo la Kaskazini mwa Afrika.
Mapema Februari 11 ndege ya jeshi la Algeria ilianguka
milimani kutokana na hali mbaya ya hewa na kuua watu 77 ikiwa ni ajali mbaya
kabisa ya ndege kuikumba nchi hiyo ndani ya muongo mmoja.

0 comments:
Post a Comment