![]() |
| Askari wa Kenya katika eneo la Kainuk, kaskazini mwa nchi hiyo, Novemba 24, 2013 katika mojawapo ya operesheni za uokozi. |
Ripoti kutoka kaskazini mwa Kenya zinasema kuwa watu
kadhaa wameuawa katika wiki ya mapambano kati ya makundi hasimu ya kikabila.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka eneo hilo, kwa uchache watu
27 wameshapoteza maisha na zaidi ya 32,000 kukosa makazi kwa zaidi ya wiki moja
sasa.
Gazeti la Kenya, la Standard Digital, limeripoti kuwa
mapambano makali yalikuwa yakiendelea katika mji wa mpakani wa Moyale. Familia nyingi
zimelazimika kukimbilia nchini Ethiopia.
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini humo limesema kuwa
jamii zilizokosa makazi zinatoka katika maeneo ya Butiye, Arosa na Gurumesa mjini
Moyale.
"Watu kadhaa wameyakimbia makazi yao tangu Jumanne
wiki hii baada ya mapigano kuongezeka. Baadhi walilazimika kukimbilia kwa ndugu
zao katika miji ya Wajir na Marsabit. Watu hawa wanahitaji msaada wa chakula,
makazi, maji, vyombo vya kupikia, nguo na vyandarua,” alisema mratibu wa
shirika hilo katika mji wa Moyale Stephen Bonaya.
Serikali ya Kenya imeagiza kupelekwa kwa wanajeshi
katika eneo hilo, huku wakazi wakiamini kuwa polisi walitoa mwanya watu hao
wenye silaha wa kupigana mpaka walipoishiwa risasi ndipo wakaja.
Nchini Kenya kumekuwepo na mapigano mengi ya kikabili
ambayo husababishwa na kugombania maji na malisho, jambo linalosababisha kuwepo
kwa mashambulizi ya mara kwa mara ya kulipiza kisasi.

0 comments:
Post a Comment