TAMKO LA KIKAO CHA MKOA –
CHADEMA, PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MAJIMBO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA
ya Kujadili na Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani
Kigoma 5/12/2013
- Ambapo atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma
kwa mikutano si chini ya miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho,
jioni Mkutano ufanyike makao Makuu ya Jimbo.
Lengo likiwa ni kuangalia uhai wa
chama.- Mambo makuu na muhimu yaliyozingatiwa:
- Usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la
Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe. Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.
- Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali
ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao.Baada ya Tafakuri ya kina na ya
Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo:-
i. Mkoa uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele
tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda
na Taifa uweze kwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi
wetu juu ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu
yetu. Hata kama yanamaumivu ….katiba yetu ifuatwe katika kutatua tatizo – Maoni
ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya k/kuu ambayo
dhahiri yalilenga kumilika Zitto – Kisiasa.
ii. Mkoa ulitishika na vitisho baada ya kupokea
taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ya mkoa kuwa hali ya usalama si
nzuri kwa ujio wa kiongozi wetu Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati
wanachama na wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo
usalama.
iii. Kwa hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata
maoni toka katika majimbo 6 kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu
asogeze mbele ziara yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na
viongozi wake Kitaifa.
iv. Hivyo Mkoa kupitia kikao hicho kuwa ni bora
kuzuia kuliko kutibu, tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa
majimbo kutofautiana mitazamo ni HATARI katika hali hiyo. Mkoa ulijiridhisha
usalama hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo
salama tu.
v. HOFU/TAHADHARI - Endapo hali haitokuwa salama
Mungu apishe mbali.
Mkoa hautokwepa lawama na Uzembe wa makusudi kwani
wajibu wa ngazi ya chini ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu.
Hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa Taifa.
LENGO KUU: NI KUHAKIKISHA
CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA
Asanteni
ALHAJ. JAFARI KASISIKO MSAFIRI WAMALWA
M/KITI MKOA 01/DEC.2013
ALHAJ. JAFARI KASISIKO MSAFIRI WAMALWA
M/KITI MKOA 01/DEC.2013
KATIBU MKOA
0756439200 0786448443
0714439200 0756448442
CHADEMA MKOA KIGOMA
0756439200 0786448443
0714439200 0756448442
CHADEMA MKOA KIGOMA
0 comments:
Post a Comment