·
Vuguvugu la Hizbullah la nchini Lebanon limesema kuwa
mmoja wa makamanda wake, Hassan al-Laqqis ameuawa asubuhi ya leo nyumbani kwake
karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Beirut.
Katika taarifa yake iliyosomwa leo katika kituo cha
televisheni cha al-Manar cha nchini humo, kundi hilo limesema kuwa kamanda huyo
aliuawa katika mji wa Hadath yalipokuwa makazi yake, limeilaumu Israeli kuwa
ndiyo iliyotekeleza mauaji hayo.
"Lawama za moja kwa moja tunaelekezwa kwa adui yetu
Israeli ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ikijaribu kumuua ndugu yetu na katika
maeneo mbalimbali lakini mara zote ilishindwa, mpaka jana jioni,” ilisema
taarifa hiyo ya Hizbullah.
"Adui huyu lazima abebe dhima na matokeo ya jinai
hii ya kinyama,” iliongeza taarifa hiyo.
Mpaka sasa Israeli haijatoa kauli yoyote kuhusu madai na
tuhuma hizo zilizoelekezwa kwake kutoka upande wa Hizbullah.
Hata hivyo, kundi moja nchini Lebanon limeelezea kuwa
limehusika na mauaji hayo.
Itakumbukwa kuwa utawala wa Israeli uliishambulia
Lebanon katika vita mbili za mwaka 2000 na 2006. Watu wapatao 1,200, wengi wao
wakiwa raia wa kawaida, waliuawa katika vita ya mwaka 2006 iliyodumu kwa muda
wa siku 33.
Hata hivyo, katika matukio yote mawili vikosi vya
Israeli vilishindwa kutimiza malengo yake na kurejea nyuma.
Mwezi Agosti 2012, katibu mkuu wa Hizbullah, Seyyed
Hassan Nasrallah, alisema kuwa kundi lake lina uwezo na ujasiri wa kuitetea
Lebanon na kwamba makombora yake yapo tayari kujibu shambulizi lolote
litakalofanywa na Israeli dhidi ya Lebanon.

0 comments:
Post a Comment