
NYOTA maarufu wa muvi za “Fast and the Furious”,
amefariki katika ajali ya gari Kusini mwa California.
Kwa mujibu wa ujumbe kutoka kwenye akaunti yake ya
Twitter, Walker, aliyekuwa na umri wa miaka 40, ambaye ameonekana katika sehemu
tano kati ya sita za filamu hizo zinazohusu matendo ya kihalifu mtaani, alipata
ajali wakati akisafiri katika gari ya rafiki yake na alikuwa akielekea kwenye
tukio moja la hisani.
“Kwa masikitiko makubwa, ninathibitisha kuwa Paul amefariki
dunia mchana wa leo katika ajali ya gari,” msemaji wa Walker, Ame Van Iden, alisema
katika barua pepe.
Polisi ya mji wa Los Angeles imetoa taarifa ikisema kuwa
watu wawili walikufa katika ajali ya gari katika eneo la Valencia, na
walipofika katika eneo la tukio walikuta gari ikiwa imezungukwa na moto. Ilitangazwa
kuwa wahusika walifariki dunia hapo hapo.
Katika movi hiyo ya “Fast and Furious” yenye mfululizo kadhaa,
nyota huyo amecheza kama Brian O'Conner akiwa kama afisa wa polisi.
Kampuni ya Universal imesema katika taarifa kuwa sehemu
ya kwanza ya muvi hiyo, ilitolewa mwaka 2001, na mauti yamemkuta huku sehemu ya
saba ikiwa inaendelea.

Kwa mojibu wa tovuti ya IMDb.com, Paul William Walker IV
alizaliwa mjini Glendale, California, mwaka 1973 na kuanza kucheza filamu
katika umri mdogo sana na kuonekana katika matangazo mbalimbali ya biashara.
Katika muvi ya “Monster in the Closet” ilitoka mwaka
1987 alicheza kama Professor Bennet na kuigiza kama nyota katika muvi ya “Throb”.
Alishiriki katika vipindi mbalimbali maarufu vya
televisheni na kuonekana katika filamu mbalimbali kama vile “Timeline,” “Into
the Blue,” “The Lazarus Project”, “Hours,” ambayo itatoka mwezi huu wa Desemba
na nyingine nyingi.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo ya IMDb, Walker ameacha mtoto
mmoja wa kike aitwaye Meadow.
0 comments:
Post a Comment