![]() |
| Waandamanaji nchini Tunisia |
Waandamanaji nchini Tunisia wamezichoma moto ofisi za
chama tawala cha Annahda katika mji wa Qafsa, katikati mwa nchi hiyo.
Waandamanaji hao walizichoma ofisi hizo baada ya
kujaribu kuingia katika ofisi za mkuu wa mkoa huo.
Polisi walifanikiwa kuwafukuza, lakini tayari walikuwa
wameshachukua makabrasha na samani za ofisi na kuzichoma moto barabarani.
Tukio hilo lilifuatia maandamano makubwa katika mji hu
ona miji mingine kama Gabes na Siliana, ambayo yaliitishwa kupinga umasikini na
ukosefu wa maendeleo.
Novemba 15, waandamanaji walikusanyika katika mji mkuu
wa nchi hiyo wakitaka chama tawala kiondoke madarakani.
Baada ya miezi kadhaa ya mgogoro wa kisiasa, chama
tawala na upinzani walianzisha mazungumzo Oktoba 25 ili kuunda serikali ya
mpito inayoundwa na watu huru wasiogemea upande wowote ambayo ingeiongoza nchi
hiyo mpaka uchaguzi ujao.
Tunisia imekuwa katika mgogoro tangu mapinduzi ya mwaka
2011 yaliyomng’oa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo, Zainul Abideen bin
Ali/
Hali hiyo ilizidi kuwa mbaya baada ya watu wenye silaha
kuwa kumuua kiongozi maarufu wa upinzani, Muhammad Brahmi, mwezi Julai baada ya
kiongozi mwenzake Chokri Belaid, kuuawa mwezi Februari.
Hali mbaya ya kiuchumi, kama ilivyo katika nchi nyingi
za Kiafrika, ni miongoni mwa vichocheo vya ghasia hizo, ambapo mfumko wa bei
unakadiriwa kufikia asilimia 6 na nakisi ya bajeti ni asilimia 7.4 ya mapato ya
ndani.

0 comments:
Post a Comment