![]() |
| Mlima Merapi, Indonesia |
Na Kabuga Kanyegeri
MFULULIZO wa milipuko ya volkano imewahamisha watu wapatao 5,000
kutoka katika vijiji saba magharibi mwa Indonesia.
Watu wanaoishi umbali wa kilometa tatu (maili1.9) kutoka eneo la
volkano wamehamishwa kutoka kwenye nyumba na makazi yao.
Kwa mujibu wa wakala wa kitaifa wa kushughulikia majanga nchini
humo, Mlima Sinabung ulioko kaskazini
mwa kisiwa cha Sumatra umekuwa ukitema majivu mekundu yenye joto, mawe na lava
nyingi na nzito na kuirusha juu umbali wa kilometa 7 (4 maili) tangu mwanzoni
mwa mwezi huu wa Novemba.
Indonesia ni eneo lenye wingi wa volkano hai na ipo katika
ukanda unaojulikana kama “Ulingo wa Moto” (Ring of Fire) uliopo baina ya Bahari
ya Pacific na Bahari ya Hindi.
Mwaka 2010, zaidi ya watu 350 walipoteza maisha yao kufuatia
mfululizo wa milipuko ya volkano katika Mlima Merapi katikati mwa eneo la Java.

0 comments:
Post a Comment