![]() |
Picha iliyotolewa Novemba
12, 2013 na Kituo cha Habari cha Umoja wa Afrika ikionesha hali ya mafuriko
katika mji wa Jowhar.
|
WATU wapatao 300 wanahofiwa kupoteza maisha katika jimbo la Putland, kaskazini mashariki mwa Somalia, kufuatia tufani kali na mafuriko makubwa yaliyolirikisa jimbo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya serikali iliyotolewa leo, mvua
kubwa, upepo mkali na mafuriko vimesababisha hali ya hatari, ambapo watu 300
wanahofiwa kupoteza maisha, mamia wengine hawajulikani walipo, mifugo mingi
imepotea, vijiji, makazi na majengo vimeharibiwa vibaya.
İdadi hiyo ya vifo haijathibitishwa na duru huru; hata
hivyo, wataalamu wa masuala ya hali ya hewa kutoka Shirika la Kimataifa
linaloshughulika na Chakula na Kilimo (FAO) wamesema kuwa mafuriko hayo nim
abaya sana.
"Puntland ni jimbo kavu, na mvua hainyeshi sana,
lakini ikinyesha kwa kiwango tunachokiona sasa, athari yake huwa mbaya sana,”
alisema Hussein Gadain, mshauri wa ufundi kutoka FAO.
Shirika la Chakula Duniani (WFP) limesema kuwa linafanya
kazi na maafisa wa jimbo hilo kutathmini mahitaji ili kujaribu kuwahudumia watu
walioathiriwa na tufani hiyo iliyoanza siku ya Jumamosi.
Barabara inayounganisha mji mkuu wa jimbo la Puntland, Garowe
na mji wa bandari wa Bossaso imekatika na hivyo kukwamisha shughuli za
upelekaji misaada.
Puntland ni ngome ya maharamia wanazishambulia meli
zinazopita kwenye pwani ya jimbo hilo. İngawa jimbo hilo lina utajiri wa
nishati, lakini wakazi wake ni masikini.

0 comments:
Post a Comment