WAKIWA bado katika maumivu ya kukumbwa na gharika kubwa
iliyosababishwa na kimbunga Haiyan kilichosababisha vifo vya maelfu, Ufilipino
imekumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.8 katika kisiwa cha Bohol.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa San
Isidro, kilometa 45 kutoka mji mkubwa wa kisiwa hicho, wa Tagbilaran, wenye
wakazi 100,000.
Taarifa kutoka Taasisi ya Volkanolojia na Seismolojia ya
nchi hiyo imesema kuwa tetemeko hilo lilipiga kilometa 70 kutoka chini ya
ardhi.
Hakuna maafa yaliyoripotiwa na mamlaka hazijatoa
tahadhari ya tsunami kufuatia tetemeko hilo.
Mwezi uliopita, tetemeko liliua watu 22 na wengine
maelfu kukosa makazi. Vilevile lilisababisha uharibifu wa zaidi ya nyumba
73,000.
Kisiwa cha Bohol kipo kusini mwa eneo lililopitiwa na
kimbunga kikali cha Haiyan, ambacho nchini humo kinajulikana kama Kimbunga
Yolanda.
Kimbunga hicho, ambacho ndio kikubwa zaidi kuikumba nchi
hiyo kwa miongo kadhaa, kilisababisha vifo vya zaidi ya watu 20,000 na kubomoa
maelfu ya nyumba. Serikali ya nchi hiyo imetengaza hali ya janga la kitaifa
huku juhudi za uokozi zikiendelea.

0 comments:
Post a Comment