![]() |
| Picha iliyopigwa Novemba 1, 2013, ikionesha mabaki ya msikiti katika manispaa ya Viana, katika mji mkuu wa Angola, Luanda |
Serikali ya Angola imekosolewa vikali na wanaharakati wa
haki za binadamu kufuatia ripoti kwamba imeipiga marufuku dini ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa ripoti moja iliyochapishwa na gazeti la the Guardian jana alhamisi, taasisi ya
Islamic Communiti of Angola (ICA) imesema kuwa misikiti 8 imebomolewa tokea
mwaka 2011, na kuongeza kuwa mtu anayeutekeleza Uislamu anakabiliwa na hatari
ya kukutwa na hatia ya kukiuka sheria za Angola.
“Kutokana na nilivyosikia, Angola ndio nchi ya kwanza
duniani ambayo imeamua kuupiga marufuku Uislamu,” alisema mkurugenze wa shirika
la Open Society Initiative of Southern Africa (OSISA) nchini humo, Elias Isaac.
“Huu ni wendawazimu. Serikali imeshindwa kuvumilia uwepo
wa mirengo mbalimbali.”
Mwezi Oktoba, Wizara ya Sheria nchini humo iliyakataa
maombi ya usajili wa Jumuiya ya Waislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa sheria ya Angola, taasisi, jumuiya au
kundi lolote la kidini linatakiwa kuwa na wanachama wasiopungua 100,000 na
lazima iwepo katika mikoa 12 kati ya 18 ili iweze kupata usajili wa kisheria
unaoiwezesha kupata haki ya kujenga shule na nyumba za ibada.
Angola inakadiriwa kuwa na Waislamu 90,000 kati ya raia
milioni 18 wa nchi hiyo.
Rais wa Jumuiya hiyo ya ICA (Islamic Community of
Angola) Dawoud Ja, alisema jana kuwa kuna misikiti isiyopungua 80 nchini Angola
ambayo imefungwa au kuvunjwa kwa sababu haina vibali, isipokuwa kwa misikiti
iliyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Luanda.
“Misikiti mjini Luanda ilitakiwa kufungwa jana lakini
kwa sababu ya kelele zilizlopigwa ulimwenguni kote kuwa Angola imeupiga
marufuku Uislamu, serikali iliamua kucha,” alisema Dawoud.
Dawoud aliongeza kuwa serikali ya Angola ilianza kufunga
misikiti miaka mitatu iliyopita, ukiwemo ule uliochomwa moto katika mkoa wa
Huambo.
Anasema kuwa msikiti mwingine ulibomolewa mjini Luanda
na nakala 120 kuchomwa moto, na Waislamu wametakiwa kuivunja misikiti wao
wenyewe.
“Huwa wanatuletea barua ya kututaka kuvunja jengo husika
na ndani ya saa 73. Inaposhindikana kufanya hivyo mamlaka za serikali yenyewe zinakuja
kutekeleza swala hilo.”
Vilevile, rais huyo wa ICA anasema kuwa wanawake wa
Kiislamu wanaovaa niqab(kitambaa cha kuficha uso) hupata madhila nchini Angola.
“Kwa hali ilivyo, wanawake wengi wa Kiislamu wanaogopa
kuvaa hijabu na niqab. Mwanamke mmoja alishambuliwa hospitalini mjini Luanda
kwa kuvaa niqab, na katika tukio lingine, binti wa Kiislamu alipigwa na
kuambiwa aondoke nchini kwa sababu alikuwa amevaa hijabu,” anasema Dawoud Ja.
KAULI YA SERIKALI
Maafisa wa serikali wanadai kuwa ripoti zilizotolewa na
vyombo vya habari kuhusu kuupiga marufu Uislamu zimetiwa chumvi na kwamba
hakuna nyumba za ibada zilizolengwa nchini humo.
“Angola hakuna vita dhidi ya Uislamu au dini nyingine
yoyote ile,” mkurugenzi wa masuala ya dini kwenye Wizara ya Utamaduni ya nchi
hiyo, Manuel Fernando, alisema na kuongeza kuwa, “hakuna agizo la serikali
linaloagiza kubomolewa au kufungwa kwa maeneo ya ibada ya aina yoyote ile.”
MWANAHARAKATI ATHIBITISHA
Hata hivyo, mwanaharakati na mwandishi wa habari za
uchunguzi nchini Angola, Rafael Marques
de Morais, amethibitisha madai yaliyotolewa na ICA (Islamic Community of
Angola) kuwa ni madai ya kweli. “Nimeliona agizo linalosema kuwa Waislamu
wabomoe misikiti wao wenyewe waondoa vifusi, la sivyo watatozwa gharama ya
uvunjanji.”
CHANZO: Press Tv

0 comments:
Post a Comment