Ayubu Mnazi Alphonce(24) ni kijana ambaye amelazwa
katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya
kuamua kuukata uume wake kwa kutumia wembe mpya ili kuepukana na usumbufu
anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa nao kimapenzi...
Imeelezwa kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na
mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika,Ayoub aliamua kuingia ndani na
kuukata uume wake kwa kutumia wembe mkali na kisha kuutupa nje..
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba mzazi
wa Ayubu baada ya kubaini kuwa mtoto wake alikuwa amejifungia chumbani kwa muda
mrefu, aliamua kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo
alipogundua ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo kikubwa cha
Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru lilifunguliwa.
Hata hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha
ya kuwa amejikata na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa
kufikishwa mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu
za msingi.
CHANZO:
Jamii Forums

0 comments:
Post a Comment