
MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye pia ni
Mhadhiri Mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo
Mvungi, usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana na kukatwa
mapanga maeneo mbalimbali mwilini ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai ya
kutaka awapatie fedha.
Watu hao walitimiza lengo lao hilo baada ya Dk. Mvungi
kuwaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.
Mtoto mkubwa wa Dk. Mvungi aitwaye Dk. Natujwa Mvungi
ameeleza kuwa baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka,
walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani ambapo
amepatiwa huduma ya kwanza kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
ambapo baadaye alipelekwa kwenye wodi katika Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa ajili
ya matibabu.
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.
0 comments:
Post a Comment