![]() |
| Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan |
Magavana 7 katika majimbo saba yenye nguvu nchini
Nigeria wamejiunga katika muungano mpya wa upinzani na hivyo kumpa wakati mgumu
Rais Goodluck Jonathan katika mbio zake za kutaka kuchaguliwa katika uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015.
Chama kikuu cha upinzani nchini humo cha All
Progressives Congress (APC), kimetangaza kuwa magavana wa majimbo saba
wamejiunga na chama hicho, ingawa kuna ripoti zinazoashiria kuwa magavana
wawili au watatu bado hawajaamua kujiunga na upinzani.
Wakati huohuo, chama cha Rais Jonathan cha Peoples
Democratic Party (PDP) kimesema kuwa hatua ya magavana hao ni hatua chanya kwa
sababu imeondosha hali ya mvurugano ambayo ingetokea ndani ya chama.
Mwezi Septemba, Rais Jonathan aliwatimua mawaziri tisa
kutokana na mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho tawala.
Magavana hao saba pamoja na mgombea wa zamani wa kiti
cha urais, Atiku Abubakar, aliyejiondoa katika chama cha Rais Jonathan Agosti
mwaka huu, wameunda mmungano wa upinzani ili kumuwezesha kugombea tena katika
uchaguzi ujao wa mwaka 2015.
Kwa sasa chama hicho cha upinzani cha APC kinadhibiti
majimbo 17 yenye wapiga kura milioni 33 waliojiandikisha, huku chama tawala cha
PDP kikidhibiti majimbo 15 tu yenye wapiga kura milioni 26 waliojiandikisha.
Rais Jonathan alichaguliwa tena mwaka 2011, kufuatia
kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Umar Yar Adua mwaka 2010.

0 comments:
Post a Comment