
Leo Oktoba 29 Uturuki inaandika historia katika sekta ya
maendeleo, hasa miundombinu kwa kuzindua mradi mkubwa wa usafiri, unaojulikana
kama Marmaray. Mradi huu utakuwa
kiunganishi cha pande mbili za mji wa Istanbul, uke wa Ulaya na wa Asia kupitia
treini ya abiria ya chini ya bahari.
Itakumbukwa kuwa mji wa Istanbul ndio mji pekee duniani
unaopatikana kwenye mabara mawili, Asia na Ulaya kwa pande hizo mbili
kutengenishwa na mkondo maarufu wa Phosphorous.
Mradi huu unaozinduliwa leo ni utekelezaji wa ndoto ya
kiongozi mmoja wa dola ya Kiuthmaniya miaka 153 iliyopita.
Mradi huu utakaozinduliwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo,
Recep Teyyip Erdogan, unalenga kuondoa tatizo la msongamano barabarani katika
mji huo na kupunguza muda wa kusafiri baina ya pande hizo mbili za mji. Marmaray,
ambayo ndio njia ya kwanza ya chini ya bahari duniani kuyaunganisha mabara
mawili, itabeba abiria 75,000 kwa saa na karibu wasafiri milioni 1 kwa siku.

Marmaray itakuwa kiunganishi baina ya mabara hayo kwa
njia ya chini ya bahari itakayopita jirani kabisa na Mkondo wa Bosporus
unaoziunganisha Bahari Nyeusi (Black Sea) na Bahari ya Marmara na kuelekea
kwenye Bahari ya Meditterania.
Njia ya Marmaray itakuwa na stesheni tatu za chini ya ardhi katika manispaa za Yenikapı,
Sirkeci na Üsküdar na vituo 36 juu ya ardhi.
Ni muhimu kuashiria hapa kuwa mpaka mwaka 2020 Uturuki inapanga
kuwa kati ya nchi 10 tajiri duniani.
Aidha, Uturuki inafanya maendeleo makubwa sana katika
sekta mbalimbali ikiwa haina maliasili kama madini, mbunga za wanyama, misitu,
mafuta, gesi na kadhalika. Bali rasilimali watu ndiyo imewafikisha huko na
uzalendo wa wananchi wake.
0 comments:
Post a Comment