SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwaarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 06 hadi 18 Agosti, na tarehe 16 hadi 19 Septemba 2013 kuwa Orodha ya Majina ya waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi yatawekwa kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kesho asubuhi tarehe 30/10/2013.
Wale watakaoona majina yao wanatakiwa kuripoti kwa Waajiri kama ilivyooneshwa katika tangazo kwa muda ambao umeainishwa katika barua zao za kupangiwa vituo vya kazi.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma 29 Octoba, 2013.

0 comments:
Post a Comment