WATANZANIA WAKAMATWA NCHINI KENYA KWA UTENGENEZAJI WA DAWA ZA KULEVYA



Polisi ya Kenya imewakamata Watanzania wawili, Wakenya watatu na Wahindi wawili kwa tuhuma ya kutengeneza madawa aina ya crystal methamphetamine jijini Nairobi, gazeti la The Standard la Kenya limeripoti leo Jumapili tarehe 1 Septemba).

Watuhumiwa walikamatwa kwa kumiliki kilogramu 50 za madawa haramu na yanakadiriwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 2 (dola milioni 1.2), gazeti la The Citizen la Tanzania liliripoti.

Watanzania Rumishaeli Mamkuu Shoo, miaka 27, na January Gabriel Liundi, miaka 30, walikamatwa Alhamisi katika gari lililobeba kifaa cha kutengenezea dawa za kulevya na malighafi za madawa. Washukiwa kutoka Kenya na India walikamatwa katika Eneo la Biashara la Cape, katika majengo ambayo yamebadilishwa kuwa maabara ya kutengeneza dawa za kulevya, kwa mujibu wa Naibu mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai Gideon Kimilu.

Inaaminika washukiwa hao ni sehemu ya ushirika ambao unatengeneza dawa za kulevya nchini Kenya na kuyasafirisha kwenda Afrika Kusini. Watafikishwa mahakamani Jumatatu.


CHANZO: Sabahi online
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment