
MAHAKAMA moja nchini Ufaransa imeamuru kuachiliwa huru
kwa aliyewahi kuwa kanali wa jeshi anayetafutwa na Rwanda kuhusiana na mauaji
ya kimbari yaliyoikumba nchi hiyo mwaka 1994.
Mahakama hiyo iliyopo katika mji wa Douai, kasikazini
mwa Ufarsana, jana iliagiza kuachiwa huru kwa Laurent Serubuga na kulitupilia
mbali ombi lililotolewa na Rwanda la kutaka mshukiwa huyo apelekwe kujibu
mashitaka nchini Rwanda.
Mahakama hiyo ilisema kuwa kanali huyo wa zamani hawezi
kushitakiwa kwa uhalifu huo kwa kuwa haukuingizwa katika sheria ya uhalifu ya
Rwanda wakati vurugu hizo zikitokea.
Aidha, mahakama hiyo iliyatupilia mbali mashitaka
yaliyotolewa dhidi ya Serubuga, ikisema kuwa kibali cha kukamatwa kilitolewa
zaidi ya miaka 10 baada ya mauaji hayo ya kimbari.
naye Mkuu wa Muungano wa Jumuiya za Kiraia nchini
Rwanda, Alain Gautier, alielezea kusikitishwa kwake, akisema kuwa Serubuga
alikuwa “mtu muhimu katika mauaji ya kimbari.”
“Ni uamuzi wa kusikitisha sana. ni mara ya 15 au 16
Ufaransa ikikataa kuwarudisha Rwanda washukiwa wa mauaji,” alisema.
Serubuga alikamatwa mwezi Julai katika mji wa Cambrai
ulio kaskazini mwa Ufaransa kwa hati ya kimataifa iliyotolewa na Rwanda.
Serubaga mwenye umri wa miaka 75, aliwahi kuwa naibu
mkuu wa majeshi wa Rwanda wakati wa mauaji ya Kimbari ya 1994, ambapo kabila la
Wahutu liliwahua watu wapatao 800,000, wengi wao wakiwa Watutsi.
Mauaji hayo yalitokea baada ya ndege iliyokuwa imembeba
Rais wa Rwanda wa wakati huo, Juvenal Habyarimana, kuripuliwa mnamo Aprili 6,
1994. Mauaji hayo yalidumu kwa siku 100 na hivyo kujulikana kama “Siku 100 za
Jahanamu.”
Mwaka 2011, Kanali Theoneste Bagosora, alielezewa na
mahakama ya kimataifa kuhusu Rwanda kama mpangaji wa mauaji ya kimbari na
kuhukumiwa adhabu ya miaka 35 jela.
0 comments:
Post a Comment