Mshambuliaji wa Yanga SC, Didier Kavumbangu akiruka
kupiga kichwa mbele ya mabeki wa Mbeya City leo Uwanja wa Sokoine.
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea leo kwenye
viwanja tofauti, huku mabingwa watetezi, Yanga SC wakilazimishwa sare ya 1-1 na
wenyeji Mbeya City na Simba SC wakishinda 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, wakati
Azam FC imetoa sare ya 1-1 na wenyeji Kagera Sugar.
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, mabingwa watetezi
walilazimika kusubiri hadi dakika ya 82 kujihakikishia japo kupata pointi moja
mbele ya Mbeya City.
Mbeya inayofundishwa na Juma Mwambusi, ndiyo walioanza
mchezo huo kwa kasi wakishambulia zaidi kutokea pembeni na kulitia misukosuko
lango la Yanga SC.
Pamoja na kocha Mholanzi, Ernie Brandts kuanzisha
washambuliaji watatu, Didier Kavumbangu, Hussein Javu na Said Bahanuzi, lakini
kuzidiwa kwa timu yao katika safu ya kiungo kuliwafanya wasiwe na madhara.
Hata hivyo, hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa
kuona lango la mwenzake na kipindi cha pili, Mbeya waliingia kwa kasi zaidi na
kufanikiwa kupata bao dakika ya nne tu tangu kuanza kipindi hicho.
Krosi maridadi ya Hassan Mwasapili kutoka wingi ya
kushoto iliunganishwa vizuri kwa kichwa na Mwagane Yeya ‘Morgan’ na kumpita kipa
Ally Mustafa ‘Barthez’ kama amesimama.
Baada ya bao hilo, Yanga walicharuka na kuanza kucheza
kwa nguvu na kushambulia zaidi na almanusra mchezo uingie dosari dakika ya 58,
baada ya Didier Kavumbangu kuuwahi mpira aliokuwa akiuchezea kipa wa Mbeya
City, David Burhan na kuutumbukzia nyavuni, lakini refa akakataa bao.
Kipa huyo alidaka shuti la Nizar Khalfan na kuanza
kuuchezea mpira kwa madaha akiudundaduna huku ameinama, ndipo Kavumbangu
akamsogelea na kwa mchecheto mpira ukamtoka kipa huyo mikononi na mshambuliaji
huyo wa Yanga akawahi kuusukumia nyavuni.
Baada ya refa Andrew Shamba kukataa bao hilo, wachezaji
wa Yanga walimtia kashikashi kidogo, kabla ya kuendelea na mchezo.
Timu ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini
mabadiliko yaliyofanywa na kocha Brandts kuwaingiza mfululizo Jerry Tegete na
Oscar Joshua kuchukua nafasi za Nizar na Bahanuzi kuliongeza uhai Yanga na
matunda yake ni kusawazisha bao dakika ya 82 kupitia kwa Kavumbangu, akimalizia
krosi David Luhende.
Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha pointi tano baada ya
kucheza mechi tatu, ikitoa sare mbili na kushinda moja, sawa na Mbeya City
ambao pia wana pointi tano sasa baada ya sare mbili na kushinda mechi moja,
zote nyumbani.
Mapema mashabiki wa Mbeya City walilitupia mawe basi la Yanga
wakati linaingia uwanjani na kusababisha kioo cha mbele upande wa dereva
kuvunjika na pia kumjeruhi dereva huyo.
Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji alikuwa jukwaani
kushuhudia mchezo huo pamoja Makamu Mwenyekiti wake, Clement Sanga na Wajumbe
wa Kamati ya Utendaji, Isaac Chanji na Mussa Katabro.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’,
Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani
Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan/Jerry Tegete dk59, Frank Domayo, Didier Kavumbangu,
Hussein Javu na Said Bahanuzi/Oscar Joshua dk59.
Mbeya City; David Burhan, John Kabanda, Hassan
Mwasapili, Deogratius Julius, Antony Matogolo, Yohana Morris, Mwagane Yeya,
Steven Mazanda, Paul Nonga/Fidelis Castor dk82, Deus Kaseke, Yussuf
Willson/Alex Sethi dk 59.
Katika mechi nyingine za Ligi hiyo, Simba SC
iliiendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza Mtibwa Sugar 2-0.
Hadi mapumziko, hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao na
kipindi cha pili, ndipo Wekundu wa Msimbazi walipong’ara, Henry Joseph akianza
kufunga dakika ya 70 na Betram Mombeki akafuatia dakika ya 90.
Simba SC; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa
Rashid ‘Baba Ubaya’, Kaze Gilbert, Joseph Owino, Jonas Mkude, Twaha
Ibrahim/Betram Mombeki dk64, Said Ndemla/Henry Joseph dk55, Amisi Tambwe, Amri
Kiemba na Haroun Chanongo/Ramadhan Singano dk77.
Mtibwa Sugar; Hussein Sharrif ‘Casillas’, Hassan
Ramadhani, Paul George, Dickson Daudi, Salim Abdallah, Shaaban Nditi, Ally
Shomary, Masoud Mohamed/Awadh Juma dk58, Juma Luizio/Mussa Mgosi dk46, Shaaban
Kisiga/Abdallah Juma dk75na Vincent Barnabas.
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Themi Felix Buhaja
alitangulia kuifungia Kagera Sugar dakika ya 25 kabla ya Khamis Mcha ‘Vialli’
kuisawazishia Azam FC dakika ya 55.
Katika mechi nyingine Coastal Union ilitoka sare ya bila
kufungana na Tanzania Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Ruvu Shooting
iliifunga 1-0 Mgambo Shooting bao pekee la Elias Maguri dakika ya 53 Uwanja wa
Mabatini mkoani Pwani, Oljoro JKT ilitoka sare ya 1-1 Rhino Rangers Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid, Arusha, wenyeji wakilazimika kusawazisha dakika ya 27
kupitia kwa Amiri Hamad baada ya Saad Kipanga kutangulia kuwafungia wageni
dakika ya tano, wakati Ashanti United ililala 1-0 mbele ya JKT Ruvu, Uwanja wa
Azam Complex, Dar es Salaam bao pekee la Amos Mgisa dakika ya 81.
Matokeo hayo, yanamaanisha JKT Ruvu inaendelea kuongoza
Ligi Kuu kwa pointi zake tisa baada ya kushinda mechi zote tatu, ikifuatiwa na
Simba SC katika nafasi ya pili yenye pointi saba. Timu nyingi zimefungana kwa
pointi tano katika nafasi ya tatu, zikiwemo Yanga, Azam na Coastal Union.

0 comments:
Post a Comment