
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Padri Joseph Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole, Mjini Unguja, baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Padri Joseph Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa Tindikali jana na watu wasiojulikanwa, katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole, ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein, akiwafariji jamaa na
ndugu wa Padri Joseph Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, waliofika
katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa
Tindikali na Watu wasiojulikanwa jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni.
Mmoja wa Ngugu wa Padri Joseph Magamba,wa Kanisa la
Romani Katoliki Parokia ya Machui, akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, hisia zake kwa Uchungu kutokana na
kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na
kukomeshwa Vitendo kama hivyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,akifafanua jambo wakati akiwafariji jamaa na ndugu wa
Padri Joseph Magamba, wa Kanisa la
Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika kumuangalia Padri huyo aliyelazwa
katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu
wasijulikanwa jana jioni katika Mtaa wa Mlandege Mjini Unguja.
0 comments:
Post a Comment