
WAPIGANAJI wa kundi la
Al-Shabaab la Somalia, wameionya serikali ya Kenya isitumie nguvu kuingia
katika jengo la Westgate, kwa kuwa matokeo yatakuwa mabaya.
Kwa mujibu wa taarifa ya
sauti iliyotolewa na kundi hilo, Al-Shabaab wameonya kwamba watawaua mateka
wote wanaowashikilia katika jengo hilo iwapo Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) na
mashirika mengine ya usalama watajaribu kutumia nguvu kuingia kwenye jengo
hilo.
“Askari wa Israeli na Kenya
vimejaribu kuingia ndani kwa nguvu lakini hawakuweza, Mujahideen (wapiganaji)
watawaua mateka wote iwapo maadui watatumia nguvu”, alisema msemaji wa
Al-shabaab, Sheikh Ali Mahmud Rage (pichani).
Hata hivyo, vikosi vya
usalama vimeapa kuendelea na zoezi la uokozi na watafanya kila linalowezekana
hilo lisitokee.
Mpaka sasa watu 69
wameshauawa na wengine wapatao 200 wamejeruhiwa.
0 comments:
Post a Comment