MWANDISHI Jaman Osman alifanya mahojiano maalumu na
msemaji wa kundi la Al-Shabaab kuhusiana na sababu za kukishambulia kituo cha
biashara cha Westgate, mjini Nairobi.
Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya mahojiano hayo
yaliyofanywa kwa Kiingereza kwenye mtandao wa Channel4
JAMAL OSMAN: Kwa nini mlifanya shambulio?
MSEMAJI: Sababu ya kufanya shambulio ni kuwalinda watu
wetu na nchi yetu, kwa sababu Kenya ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia
sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio
walitushambulia na tunajilinda.
Haidhuru kama wewe ni Muislamu au Mkristo, sheria
inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule anayekushambulia.
JO: Mumeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza,
hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?
MSEMAJI: Tumewaambia Wakenya na wale wanaoenda Kenya
kwamba hatuwezi kuvumilia kile ambacho Kenya inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda
na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya.
Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote
aliyejiandaa kwenda Kenya lazima ajiandae kukabiliana na ukweli huo, na
hatuwaogopi watu wa Ulaya ama wa Marekani, kwa sababu sisi si dhaifu.
Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao
wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu
wao kama mnataka kuwa salama.
JO: Kwa nini mliliilenga Westgate?
MSEMAJI: Sababu ya kuielenga Westgate ni kwa kuwa
Wakenya na serikali yao wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma
watu wao Somalia, wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu,
popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo.
Sababu ya kuilenga Westgate ni kwamba, tunajua ni sehemu
ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwa sababu inaingiza pesa nyingi na ipo
katikati ya jiji.
Ni sehemu inayowaumiza zaidi na kwa sababu tulitaka
kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikie
kila Mkenya.
JO: Wapiganaji wenu ndani ya Jengo bado wanapigana?
MSEMAJI: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika
hatamu.
JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?
MSEMAJI: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.
JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini yatakuwa
matokeo ya hili?
MSEMAJI: Kama Mungu akipenda, tunategemea Wakenya
watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua
kuwa hawawezi kuishikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategee waishi kwa
amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kutuma kwao.
JO: Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni
mwanzo tu na mtaendelea, ama mumeshifikia malengo yenu?
MSEMAJI: Tunaiambia Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni
ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita
yenyewe.
JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya ni kuiacha nchi yenu
kama wanataka amani?
MSEMAJI: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa
kuaiacha nchi yetu.
JO: Kwa nini mnalenga watu wasio na hatia?
MSEMAJI: Raia wa kigeni wanatakiwa kuondoka kwenye nchi
hiyo (Kenya) kwa sababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na
tunamwambia kila mtu- Kenya ni eneo la vita.
JO: Kwa kuwa unasema raia
wa kigeni na Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani
kwao?
MSEMAJI: Tunawaambia
Waingereza, kwa kuwa tunaamini wanawasaidia Wakenya na Wakenya ni watumwa wao,
wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya walitoe jeshi lao Somalia.
Na Waingereza wanajua
Wasomali hawatakata tamaa. Tuliwakatalia Waingereza huko nyuma, ambao wana
nguvu kuliko Wakenya.
(Kwa hisani ya mashirika ya habari)
0 comments:
Post a Comment