Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Tanzania imesema kuwa
hadi kufikia leo Septemba 23, 2013 ni Mtanzania mmoja tu aliyetambulika kwa
jina la Bwana Vedastus Nsanzugwanko mwenye cheo cha Umeneja katika kitengo cha
Ulinzi wa Watoto, cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Hazina ya Kuhudumia Watoto
(Child Protection, UNICEF) ambaye taarifa zake ziliifikia Ofisi ya Balozi kuwa
amejeruhiwa kwa risasai na milipuko ya maguruneti kwenye miguu yake yote
miwili.
Taarifa hiyo inasema kuwa kwa sasa hali Bwana Vedastus
inaendelea vizuri akiwa anapatiwa matibabu alikolazwa katika hospitali ya Aga
Khan ya jijini Nairobi, Kenya.
Imetaarifiwa kuwa Ubalozi unaendelea kufuatilia kwa
lengo la kupata taarifa zaidi endapo kutakuwepo Watanzania wengine waliodhurika
katika tukio hilo.
Ofisi ya Ubalozi kwa kushirikiana na Uongozi wa Chama
cha Watanzania nchini Kenya (TWA) unaandaa utaratibu maalumu utakaowezesha TWA
kuitikia wito uliuotolewa wa kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia wahanga.
CHANZO: Jamii Forums

0 comments:
Post a Comment