Takribani robo ya wanaume sita kutoka nchi za Asia
waliohojiwa katika utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa wamekiri kufanya
ubakaji angalau mara moja.
Utafiti huo uliochapishwa Jumanne iliyopita katika
Jarida la Lancet Global Health uliwahoji
zaidi ya wanaume 10,000 katika maeneo mbalimbali ya nchi za Bangladesh, China, Cambodia, Indonesia, Sri
Lanka, na Papua New Guinea.
Karibu asilimia 10 ya waliohojiwa walisema kuwa
walifanya mapenzi ya kulazimisha na mwanamke ambaye sio mshirika wao. Lakini asilimia
hiyo ilipanda mpaka kufikia 24 pindi washirika wao walipojumuishwa katika
swali.
Takriban nusu ya wale waliokiri walieleza kuwa waliwahi
kuwabaka wanawake mbalimbali. Wengi walisema kuwa hawakukumbana na mkono wa
sheria kwa vitendo vyao hivyo.
Wachunguzi walionya kuwa uchunguzi wao hauakisi takwimu
rasmi za vitendo vya ubakaji katika nchi husika, kwa sababu ulifanyika katika
maeneo tisa tu. Hata hivyo, utafiti huo utasaidia kuhamasisha juhudi za kuzuia
vitendo vya ubakaji na dhulma dhidi ya wanawake.
Utafiti ulibaini kuwa sababu za dhulma hizo dhidi ya
wanawake zinatofautiana kutoka eneo moja kwenda jingine. Dhulma shidi ya watoto,
matumizi ya ulevi, umasikini, migogoro na vita katika maeneo husika ni miongoni
mwa sababu za vitendo hivyo.
Karibu robo tatu ya wale waliokiri kubaka walisema kuwa
walifanya hivyo kukidhi matamanio ya kimwili. Asilimia 60 walisema kuwa walibaka
kwa ajili ya burudani, huku asilimia 40 wakisema kuwa walibaka ili kumuadhibu
mwanamke husika.

0 comments:
Post a Comment