Mwimbaji wa nyimbo za Injili Jijini Nairobi,
Kenya,George Barasa maarufu kama Joji Baro amejitangaza kuwa yeye ni shoga.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 22 akizungumza na
mtandao mmoja wa nchini humo alisema kuwa alizaliwa Jijini Nairobi na baadaye
kuhamia Bungoma miaka michache baadaye.
Aidha ameongeza kuwa pamoja ya kuwa ni shoga pia
ameathirika na ugonjwa hatari wa Ukimwi pia ni mwanaharakati wa kutetea Haki za
Mashoga na Wasagaji na wana zaidi ya wanachama 2,800, Ambao wote ni mashoga na
wasagaji ambapo vijana idadi yao 15 na watu wazima ni 68.
Alisema kuwa aliamua kuhamia Mjini EMBAKASI BAADA YA
FAMILIA yake kumtenga alipojuliakana anajihusisha na vitendo hivyo.
Alipokuwa anasoma shule ya Mtakatifu Paulo Miluki High
School ndipo alipoanza kujifunza vitendo hivyo vya ushoga na kuwa na uhusiano
wa kimapenzi na kiongozi mmoja wa kanisa Katoliki.
Machi 11, 2012 , Madaktari walimpima na kugundulika kuwa
ni mwathirika wa VVU / UKIMWI na kwamba amedai kuwa kwenye muziki wa INJILI
amekuwa akipata upinzani mkubwa kutoka kwa wanamuziki mwenzake wa muziki huo.
Anasema amechoka kuhukumiwa na kuonewa huku
akinyanyapaliwa na watu wengine baada ya kugundulika kuwa nafanya vitendo
hivyo.
‘Mimi ni binadamu,Kama binadamu yeyote naumia sana
ninavyonyanyapaliwa,’ alisema Barasa.
Anasema kwenye masuala ya urembo hayuko nyuma ana mawigi
15 na zaidi ya pea za viatu virefu ‘High hills’ 30.
‘Napenda sana urembo na pia naandika kitabu cha maisha
yangu kiitwacho "Dream Boy" ambacho kitaeleza historia nzima ya
maisha yangu na jina la albanu yangua ya injili inaitwa "Bora Siku"
alisema Barasa.
‘Namtumikia Mungu na natumaini Mungu anakubali utumishi
wangu,’ alimalizia Barasa.


0 comments:
Post a Comment