![]() |
| Helikopta ya jeshi la Syria ikiwa katika uwanja wa jeshi wa Minnigh baada ya kutunguliwa |
NAIBU Waziri Mkuu wa Uturuki Bulent Arinc amewaambia
waandishi wa habari kuwa ndege za kivita za Uturuki zimeidondosha helikopta ya
jeshi la Syria baada ya kuingia katika anga yake.
Helikopta hiyo aina ya MI-17 mali ya Syria ilidondosha
katika jimbo la kusini la Hatay baada ya kupenya umbali wa kilometa 2 katika
anga ya Uturuki.
Arinc alisema huwa hapakuwa na taarifa kuhusu
kilichowakuta marubani wa helikopta hiyo kwa sababu ilienda kuangukia katika
ardhi ya Syria. Vilevile alieleza kuwa jeshi la anga la Uturuki liliionya
helikopta hiyo mara kadhaa kuondoka katika anga yake kabla ya kupigwa kwa
makombora.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa rasmi zinasema kuwa
wapiganaji wanaopigana dhidi ya serikali ya Syria wamewaua marubani hao. Pia kuna
ripoti zinazosema kuwa rubani mmoja alikamatwa na waasi huku mwingine akiwa hajulikani
aliko.
Mpaka sasa serikali ya Syria haijatoa maelezo yoyote juu
ya tukio hilo.
Tukio hilo linakuja mwaka mmoja baada ya jeshi la anga
la Syria kuidondosha ndege ya kivita ya Uturuki baada ya kuingia katika anga
yake. Inasemekana kuwa ndege hiyo ilidondokea upande wa Syria jirani na kijiji
cha Um al-Touyour. Hata hivyo, Uturuki ilisisitiza kuwa ndege yake iliingia
katika anga ya Syria lakini ikaondoka haraka baada ya kuonywa, na ilitunguliwa ikiwa
katika anga ya kimataifa dakika kadhaa baadaye.

0 comments:
Post a Comment