Al Jazeera: Ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu askari
wa Kenya walipoingia Somalia kupambana na al-Shabaab. Kwa nini Al-Shabaab
waishambulie Nairobi leo na sio kabla?
SHEIKH ABULAZIZ ABU MUSCAB: Tumechelewa kuishambulia
Nairobi. Hatufanya hivyo mapema kwa sababu walikuwa wakitarajia kuwa
tutashambulia. Lengo letu ni kumshambulia adui anapokuwa hana matarajio ya
kushambuliwa. Mara hii hawakutarajia kuwa tutawashambulia. Tulichagua muda
mzuri wa kushambulia.
AJ: Hii ni mara ya kwanza kwa Al-Shabab kuishambulia Nairobi?
SA: Hilo sio muhimu. La muhimu ni kwamba sisi ndio
tulioshambulia. Sio muhimu kusema kama tuliwahi kushambulia huko nyuma au la.
AJ: Shambulizi hili limefanyika kwenye kituo cha
Biashara cha Westgate, ambapo wakati linashambuliwa lilikuwa limejaa watu. Kwa nini
Al-Shabaab inashambulia eneo lililojaa raia?
SA: Sehemu tuliyoshambulia ni kituo cha biashara cha
Westgate. Ni mahali ambapo watalii kutoka duniani kote huja kununua vitu, ni
mhali ambapo wanadiplomasia hukutana. Ni mahali ambapo viongozi wa Kenya huenda
kupumzika na kubarizi. Westgate ni mahali ambapo kuna maduka ya Wayahudi na
Wamarekani. Hivyo, tumewashambulia.
Kuhusu vifo vya raia, Kenya ndiyo inayotakiwa kuulizwa
kwanza kwa nini waliwaua raia wa Kisomali katika makambi ya wakimbizi? Kwa nini
waliua watu wasiokuwa na hatia katika mikoa ya Gedo na Jubba. Wao ndio wanaotakiwa
kuulizwa kwanza kabla yetu.
AJ: Al-Shabab inadai kuwa inawatetea Waislamu na hususan
Wasomali. Baadhi ya watu waliouawa na kujeruhiwa katika tukio hili wanaona kuwa
hili ni kinyume na madai yenu.
SA: Historia inatuunga mkono katika madai yetu. Sisi ndio
pekee tunaowatetea Wasomali na Somalia. Sisi ndio kundi pekee linalopigana na
maadui wa muda mrefu wa Somalia. Sisi ndio pekee tunaoweza kuwaambia maadui wa
Somalia “hapana”.
Kuhusu kupotea kwa uhai wa watu, kuna askari wa Kenya
wanaofyatulia risasi wapiganaji wetu. Kuna majibishano ya risasi. Hakuna ushahidi
kwamba risasi zetu ndizo zilizowaua.
Tuliwaachia huru Waislamu wote tulipolidhibiti jengo. Mashuhuda
wametuunga mkono juu ya hili.
AJ: Unadhani shambulizi hili litaifanya Kenya iyaondoshe
majeshi yake kutoka Somalia?
SA: sisi sio tunaotakiwa kujibu hili swali. Serikali ya
Kenya ndiyo inayotakiwa kujibu. Uamuzi
wa kuwaondoa au kutowaondoa askari ni wa kwao. Wasipoondoka, mashambulizi kama
haya yatakuwa ya kawaida nchini Kenya. Iwapo hawataondoka mashambulizi kama
haya yataendelea kutokea katika miji ya Kenya kila siku.
AJ: Kabla ya majeshi ya Kenya kuingia Somalia Oktoba
2011, uhusiano wa Al-Shabaab na serikali ya Kenya ulikuwa vipi?
SA: Siku zote tulijua kwamba Kenya ni adui wa watu wa
Somalia. Tulilijua hili tulipoidhibiti mikoa ya mpakani. Tulitarajia kuwa
watatuvamia. Hatuwaamini na wao hawatuamini.
AJ: Kenya inasema kuwa itawasaka wahalifu waliotekeleza shambulizi hili na
hawatakaa mpaka wawashinde. Unasemaje kuhusu hili?
SA: Sisi sio wahalifu. Sisi tunachokifanya ni kujilinda
na kulinda haki zetu, haki za Wasomalia.
Leo hii hakuna mwenye rikodi mbaya ya uhalifu kama Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta. Anazungumzia makumi ya watu waliouawa katika jengo la
Westgate ilhali yeye ni anahusika kwa vifo vya maelfu ya watu waliouawa wakati
wa kuwania urais. Kama Wakenya wanataka kumuwajibisha mtu kwa uhalifu basi waanze
kumuwajibisha yeye kwanza.
AJ: Watu wengi, ikiwa ni pamoja na Serikali za Somalia
na Kenya, wanasema kuwa Al-Shabaab kulilenga eneo lililojaa raia ni dalili ya
udhaifu, kwamba Al-Shabaab inaishiwa nguvu na kwamba inaelekea kutoweka kabisa
na kubaki kuwa historia. Je hali iko hivyo?
SA: Ni watu gani hao wanaotuhukumu? Udhaifu wa hawa watu
unaonekana kwa kila mtu. Serikali ya Somalia inalindwa na vifaru ili iendelee
kuwa madarakani. Wakenya wanategemea msaada kutoka nje, hata kwenye
kushughulikia suala dogo kama la Westgate. Waliomba msaada kutoka Magharibi.
AJ: Mwisho, Kenya imekielezea Kituo cha Vijana cha Mombasa
Youth Centre (MYC) kwamba ni taasisi ya kigaidi. Katika maeneo mbalimbali kundi
hilo limekuwa likiwaunga mkono Al-Shabaab. Al-Shabaab ina uhusiano gani na MYC?
SA: Uhusiano kati ya MYC na sisi ni kama uhusiano uliopo
baina ya Waislamu. Wao ndugu zetu wa Kiislamu. Uhusiano uliopo ni kwamba wao ni
Waislamu na sisi ni Waislamu, wana haki kutoka kwetu kama Waislamu wengine.

0 comments:
Post a Comment