Kundi hilo la takriban watu 10-15 liliweza kuingia
kupitia lango kuu la jumba hilo huku lingine likiingia kutoka eneo la kuegeshea
magari lililoko paani.
Katika lango kuu walianza kwa kumuua mkurugenzi wa
kampuni ya usalama inayolinda eneo hilo kabla ya kuelekea paani ambapo ulikuwa
na hafla iliyoandaliwa na idhaa ya East FM.
Wale walioingilia lango kuu wakafululiza hadi duka la
Nakumatt lililoko katika jengo hilo na ni hapa ambapo mauaji ya Wakenya
wasiokuwa na hatia yoyote yalipoendelezwa zaidi.
Milio ya risasi ikasheheni angani.
Huku haya yakijiri tayari maafisa wa polisi walikuwa
wamepata habari hizo na vikosi mbali mbali vikakita kambi na kulizingira eneo
hilo, magharibi, mashariki, kusini na hadi angani.
Shughuli ya uokozi ikaanza ili kufanikiwa kuwashikilia
mateka kwa siku tatu mtawalia huku vikosi vya usalama vinajua ina maana kuwa
magaidi hawa walikuwa wamejihami vilivyo.
NI AKINA NANI HAWA ?
Duru za kuaminika zinaarifu kuwa, washukiwa hawa ni watu
wa tabaka na mataifa mbali mbali wakiwemo wafuatao wanaodaiwa kushiriki kwenye
shambulizi hilo:
1. Sayd Nuh – 25 – Kismayu
2. Ismael Galed – 23 – Finland
3. Mustafa Noordiin – 24 – Marekani
4. Abdifatah Osman- 24 – Marekani
5. Kassim Musa – 22 – Garissa
6. Mohammed Badr – 24 – Syria
Aidha waziri wa masuala ya ndani na usalama Joseph Ole
Lenku amefutilia mbali madai kuwa kiongozi wa kundi hilo ni mwanamke
akishikilia kwamba ni wanaume waliovalia mavazi ya kike.
Kufikia sasa vikosi vya kenya vya usalama vimechukua
usukani wa ghorofa zote za jengo hilo, na kulingana na Lenku ni kuwa magaidi
wangali wamejificha, japo wawili tayari wameuawa.

0 comments:
Post a Comment