KURA za maoni zinaonesha kuwa chama cha Kansela wa
Ujerumani, Angela Merkel, kinatarajiwa kupata ushidni mkubwa katika viti vya
bunge katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Tathmini zilizofanywa na vituo vya televisheni leo
kuhusu maoni ya wananchi zilionesha kuwa Chama cha Markel cha Christian
Democratic Union (CDU) kitashinda viti 304 kati ya 606 katika bunge.
Hiyo ina maana kwamba muungano wake wa wahafidhina
hautahitaji washirika wengine na wanaweza kuunda serikali peke yao.
Kura za maoni za mapema zilionesha kuwa chama cha Markel
kilihitaji kuunda kile kinachoitwa muungano mkubwa na upinzani wa mrengo wa
kushoto wa Chama cha Social Democratic.
Haya yanakuja wakati Chama cha upinzani cha Alternative
fur Deutschland (AfD) kikiwa hakina uhakika wa kuingia bungeni. Maoni ya sasa
yanaonesha kuwa chama hicho hakiwezi kupata asilimia tano ya viti vyote.
Akipewa nuvu na matokeo haya, Merkel ameahidi kufanya
makubwa zaidi katika miaka mingine minne ya uongozi wake.
“Kwa pamoja tutafanya kila kitu katika miaka mingine
minne ili kuifanya kuwa yenye mafanikio kwa Ujerumani,” alisema Markel.
Wakati wa kampeni mjini Berlin jana, Merkel aliuambia
umati wa wafuasi wa chama cha Christian Democrat kuanza kukusanya nguvu tena
kutoka kwa raia wa Ujerumani.
“Mimi binafsi ninawaomba wananchi wa Ujerumani: nipeni
nguvu zaidi ili niweze kuitumikia Ujerumani kwa miaka mingine minne,” alisema
Markel.
.jpg)
0 comments:
Post a Comment