![]() |
WAZIRI wa mambo ya ndani wa Tunisia amesema kuwa idadi
kadhaa ya mabinti wa Kitunisia wamekuwa wakisafiri kwenda nchini Syria na
kutumika katika shughuli za ngono kwa ajili ya makundi yanayopigana dhidi ya
serikali ya nchi hiyo.
Jana alihamisi, Waziri huyo, Lotfi Ben Jeddou aliwaambia
wabunge kuwa wanawake wa Kitunisia waliosafiri kwenda Syria wamerejea na
ujauzito kutokana na kugeuzwa kuwa washirika wa ngono kwa mamia ya wapiganaji
wa makundi hayo, kwa kile kinachoelezwa kuwa ni “jihadi ya ndoa.”
Bin Jeddo alisema kuwa wizara ya mambo ya ndani
imewapiga marufuku wanawake 6,000 wasisafiri kwenda Syria tangu Machi 2013 na
kuwatia nguvuni watuhumiwa 86 wanaotengeneza “mitandao” inayotumika
kuwasafirisha vijana wa Kitunisia kwenda kushiriki vita nchini humo.
“Walikuwa na mahusiano ya kijinsia na waasi 20, 30, 100.
Baada ya kutumika kwa kazi hiyo waliyoiita 'jihad al-nikah' - (jihad ya ndoa) –
wanarudi nyumbani wakiwa wajawazito,” alisema Ben Jeddou.
Waziri huyo hakusema ni wanawake wangapi walioenda
Syria, lakini ripoti za vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa ni mamia
ya wanawake.
Aidha, waziri huyo aliyakosoa vikali makundi ya haki za
kibinaadamu yanayoukosoa uamuzi wa serikali kuwapiga marufuku wale wanaosafiri
kwenda Syria kupigana vita. Vijana wengi waliokumbwa na marufuku hiyo ni wale
walio chini ya umri wa miaka 35.
“Vijana wetu wanawekwa msitari wa mbele wa mapambano na
wanafundsihwa jinsi ya kuiba na kuvamia vijiji,” alisema Bin Jeddo.
Naye Mufti wa zamani wa Tunisia, Sheikh Othman Battikh, mnamo
tarehe 13 Aprili alisema kuwa mabinti wa Kitunisia walikuwa “wakihadaiwa” kwenda Syria kutoa huduma za ngono kwa waasi
wanaopambana kuundoa utawala wa Rais Bashar al-Assad.
Mufti huyo, ambaye baadaye aliondolewa kwenye wadhifa
wake, aliielezea hiyo inayoitwa “jihadi ya ngono” kuwa ni aina ya ukahaba.
“Sasa hivi wanawasukuma mabinti kwenda Syria kwa ajili
ya Jihad. Mabinti wadogo 13 wamepelekwa kwa ajili ya huduma ya ngono. Hiki ni
kitu gani? Huu ni ukahaba. Ni uharibifu wa kimaadili,” alisema mufti huyo
wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mwezi Agosti mwaka huu, mkurugenzi mkuu wa usalama wa
umma, Mustafa Bin Omar alisema kuwa “jihadi ya ngono” ilikuwa imeshamiri sana
magharibi mwa nchi hiyo ambapo makundi ya wapiganaji wamejichimbia.
Bin Omar aliwaambia waandishi wa habari kuwa makundi ya
wanamnagambo wanawatumia mabinti wadogo, waliojifunika nyusoni, kutoa huduma za
kijinsia kwa wapiganaji wa kiume.
CHANZO: al-Arabiya/ Mitandao ya kijamii

0 comments:
Post a Comment