Idadi ya vifo kutokana na mvua, mmomonyoko wa udongo na
mafuriko nhini Mexico imeongezeka na kufikia 97 wakati kimbunga kipya kikipiga
eneo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Taarifa rasmi iliyotolewa inasema kuwa vifo 65 vimetokea
katika jimbo la kusini magharibi la Guerrero ambalo limeathirika vibaya sana.
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa watu wapatao 2,000
wamehamishwa, nyumba 21,000 zimekatiwa umeme huku madaraja na barabara katika
jimbo hilo zikiharibiwa vibaya sana.
Hayo yanatokea wakati mawimbi mapya ya kimbunga Manuel,
ambacho kiliikumba nchi hiyo mapema wiki hii, kikipiga katika jimbo la Sinaloa
na kusababisha kijiji kidogo cha wavuvi kukimbiwa na wakazi.

0 comments:
Post a Comment