MABAO 6-0 iliyoyapata Simba Sc leo dhidi ya Mgambo
Shooting, yameiwezesha timu hiyo kufikisha poiunti 10 na hivyo kukalia usukani
wa ligi hiyo.
Aidha,mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga Sc,
wameendelea kubanwa tena mjini Mbeya baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1
dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Sokoine mjini
humo.Ikumbukukwe kuwa Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 jumamosi iliyopita dhidi ya
Mbeya City katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja huo.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba Amis Tambwe ambaye
pia ni kinara wa mabao katika ligi hiyo kwa sasa, aliiandikia mabao manne huku
Haruna Chanongo akifunga mawili.
Aidha, Wanalambalamba Azam Fc nao wamebanwa mbavu na
vibonde wa ligi hiyo Ashanti United baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 katika
mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Matokeo mengine ya ligi hiyo ni kama ifuatavyo:
Jkt Ruvu V Ruvu Shooting 0-1
Mtibwa Sugar V Mbeya City 0-0
Rhino V Coastal Union 1-1
Kagera Sugar V Jkt Oljoro 2-1

0 comments:
Post a Comment