KASISI mmoja wa Kanisa Katoliki katika jimbo la Missouri
nchini Marekani amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 5 jela kwa kutengeneza picha
na filamu za uchi za watoto.
Adhabu hiyo ilitolewa na Jaji Gary Fenner, ambapo kasisi
Shawn Ratigan, mwenye umri wa miaka 47, atatumikia kipindi kilichobaki cha
maisha yake katika jela kwa sababu katika mfumo wa jela za Marekani hakuna
msamaha wa kutoka jela ya kumaliza kifungo ambao hutolewa kwa watu kwa sharti
la kutotenda kosa.
Mwezi Agosti mwaka jana, Ratigan alikiri kosa katika
mashitaka matano ya kuzalisha au kujaribu kuzalisha filamu za uchi za watoto.
Kwa mujibu wa waendesha mashitaka, aliwapiga picha
watoto wa kike ndani na jirani na makanisa aliyokuwa akifanya kazi katika Mji
wa Kansas, Missouri.
Mwezi desemba 2010, fundi mmoja wa kompyuta alikuta
maelfu ya picha za watoto wadogo watano katika kompyuta ndogo (laptop) ya Ratigan
wakati akifanya kazi kwenye kompyuta hiyo.
Fundi hiyo alichukua uamuzi wa kuripoti kisa hicho kwa
maafisa wa Kanisa Katoliki la Mt. Joseph katika Dayosisi ya Mji wa Kansas. Hata
hivyo, Askofu Robert Finn wa Dayosisi hiyo hakuzikabidhi polisi picha hizo na aliamua
kumpeleka Ratigan kufanyiwa uchunguzi wa akili.
Matukio hayo yalisababisha Askofu Finn ashitakiwe kwa
makosa ya jinai na kumfanya kuwa afisa wa ngazi ya juu wa Kanisa Katoliki
nchini Marekani kushhitakiwa kwa makosa ya uhalifu na jinai.
Ratigan, aliwaomba msamaha waathirika na familia zao
kabla ya kuhukumiwa. Hata hivyo, alisema kuwa hakutakiwa kupewa adhabu ya
kifungo cha miaka 50 jela.
“Jela ni jehanamu. Ninajua ninastahiki adhabu ya miaka
15, lakini miaka 50? Sidhani,” alisema Ratigan.
0 comments:
Post a Comment