
WATU sabini wamepotez maisha katika mlipuko wa bomu
uliotokea nje ya kanisa moja katika mji wa kaskazini magharibi wa Peshawar
nchini Pakistan.
Maafisa wanasema kuwa shambulio hilo lilitokea katika Wilaya
ya Koshati Gati. Mabomu mawili yalilipuka wakati waamini wakitoka kwenye ibada
katika Kanisa hilo Kongwe nchini humo.
Maafisa hao wansema kuwa watu wapatao 100 wakiwemo
wanawake na watoto walijeruhiwa katika shambulizi hilo.
Hakuna kundi lililodai kuhusika, ingawa baadhi ya
makundi ya wapiganaji yamekuwa yakilaumiwa kwa mashambulizi yaliyotokea huko
nyuma dhidi ya Wakristo wachache katika taifa hilo.
Maelfu ya Wapakistan wamepoteza maisha yao katika
milipuko ya mabomu na mashambulizi mengine yanayofanywa na wanamgambo tokea
mwaka 2001, baada ya nchi hiyo kuunda ushirika na mataifa ya kigeni katika vita
dhidi ya ugaidi.
0 comments:
Post a Comment