
Ireland Kaskazini 2 - 4 Ureno
Akitaniwa kwa kuimbwa "una thamani ndogo zaidi ya Bale", Christiano Ronaldo kafunga goli tatu ndani ya dakika 15 kuipeleka Ureno juu ya kundi lao
Scotland 0 - 2 Ubelgiji
Wakali Hazard, Fellaine na wenzao wanaongoza kundi kwa pointi 5, ushindi mmoja unatosha kuwapeleka Belgium kombe la dunia
Italia 1 - 0 Bulgaria
Mabingwa wa dunia 2006 wanahitaji points 3 zaidi kufuzu kombe la dunia
Estonia 2 - 2 Uholanzi
Uholanzi yang'ang'aniwa ugenini, wanaongoza kundi kwa pointi 6
Uingrereza 4 - 0 Moldova
Ushindi mwepesi kwa Uingereza huku Dani Welbeck akipewa kadi ya njano ya magumashi, atakosa mechi muhimu jumanne dhidi ya Ukraine
Ghana 2 - 1 Zambia
Marudio ya vita kombe la mataifa ya Afrika, Ghana wameshinda na kuongoza kundi lao kwa pointi 4
Mexico 1 - 2 Honduras
Mexico wanazidi kujiwekea ugumu kufuzu.
0 comments:
Post a Comment