SIKU moja baada ya kukamatwa mtu aliyejifanya kuwa daktari bingwa katika Hosptali ya Rufaa KCMC mkoani Kilimanjaro imeelezwa kuwa tabibu katika Hospitali ya Madona ya Tabata Dar es salaam. Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA umebaini kuwa mtuhumiwa Alex Massawe (38) mkazi wa Sinza, Dar es Salaam ambaye anashikiliwa na mkoani Kilimanjaro ana taaluma ya utabibu.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alisema baada ya kufanya mahojiano ya kina na mtuhumiwa huyo, ilithibitika kuwa ana taaluma ya utabibu.
Massawe alikamatwa juzi asubuhi katika Hospitali ya KCMC akijiandaa kutoa huduma ya upasuaji kwa mgonjwa aliyekuwa na tatizo la ngozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa habari wa KCMC, , Gabriel Chisseo, daktari huyo bandia aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo baada ya baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mtu ambaye amekuwa akijitangaza kwamba ni daktari bingwa wa upasuaji.
Inadaiwa mtuhumiwa huyo alikuwa amepanga kufanyia upasuaji wa ngozi, Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo baada ya kukutana na mama yake na kumuahidi kumpatia huduma kwa malipo.
Habari za kuaminika zinasema kabla ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi wa kijana huyo, mkazi wa Manispaa ya Moshi, Pamvelina Shirima, alikutana na mtuhumiwa huyo katika baa moja maarufu mjini hapa iliyopo eneo la Dar Street na kumtaka ampe Sh. 200,000 ambazo alidai zingeharakisha mgonjwa kufanyiwa vipimo vya upasuaji.
Kamanda Boaz alisema uchunguzi unaendelea na utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
CHANZO: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment