Kwa mara nyengine tena leo hii kumetangazwa kutokea
tukio la kumwagiwa acid ambapo imeelezwa jioni hii Padri Joseph Magamba
amemwagiwa acid maeneo ya Sunshine Internet Cafe hapo Mlandege, mjini Zanzibar.
Binafsi nalaani vikali kitendo hicho cha kinyama na cha kishenzi kabisa.
Juzi tu Jumatano nilisoma katika gazeti la Mwananchi
tukio la mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi Christian Msema wa Mburahati, Dar
es Salaam kumwagiwa acid na watu wasiojulikana waliokuwamo kwenye bajaj.
Matukio haya ni ya kinyama na ya kutisha na yanaonekana
kushika kasi kila uchao. Bahati mbaya licha ya Polisi kutangaza operesheni
maalum ya kutafuta kile walichokiita mtandao wa acid hakuonekani mafanikio yoyote.
Hivi uwezo wa uchunguzi wa Jeshi la Polisi umeshuka kiasi hichi? Na kwa nini
hadi leo Serikali haijapiga marufuku uuzaji au upatikanaji mwengine wa acid
ambao unaonekana kufanyika kiholela kiasi cha kupatikana kirahisi na kutumika
kufanyia uhalifu kiasi hichi?
Yeyote au kikundi chochote kilicho nyuma ya matukio haya
kinapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na kusakwa ili kuchukuliwa hatua kali dhidi
yao.
.jpg)
0 comments:
Post a Comment