WAPALESTINA WENGINE WAZIDI KUUAWA





Wanajeshi wa utawala wa Israeli wamewapiga risasi na kuwaua Wapalestina watatu na kuwajeruhi wengine wasiopungua arobaini katika kambi ya wakimbizi ya Qalandia katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Duru za kitabibu nchini Palestina zimeripoti kuwa Robin al-Abed mwenye umri wa miaka 32 na Younis Jihad Abu al-Sheikh Jahjouh mwenye umri wa miaka 22, walifariki dunia kutokana na mjeraha ya risasi zilizofyatuliwa na vikosi vya Israeli wakati wa usiku.

Jihad Aslan, kijana mwingine wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 20, amefariki dunia leo kutokana na majeraha baada ya kuelezewa kuwa ubongo wake ulikuwa umekufa kabisa.

Mauaji hayo yalitokea baada ya askari kadhaa wa Israeli kuishambulia kambi hiyo ya wakimbizi iliyo al-Quds Mashariki (Jerusalem), kwa lengo la kumkamata mfungwa wa zamani wa kisiasa wa Palestina.

Vijana wa Kipalestina waliwarushia mawe wanajeshi hao, ambao nao walijibu kwa kufaytua risasi za moto.

Mkuu wa Kitengo cha Dharura cha Shirika la Mwezi Mwekundu mjini Ramallah,  Mohammad Samhan, amesema kuwa shirika lake lilipokea simu nyingi kuhusu idadi kubwa ya majeruhi katika kambi ya Qalandia, na kwamba magari ya wagonjwa yalifanya haraka na kuwahamishia majeruhi kwenye Kituo cha Tiba cha Palestina.

Vyanzo vya ndani vinasema kuwa mfungwa wa Kipalestina aliyeachiwa huru hivi karibuni, Yousef al-Khatib, ambaye alikaa miaka kumi katika korokoro za Israeli, alitekwa na jeshi la Israeli.

Mnamo Agosti 20, Mpalestina Majd al-Shaleh aliuawa na vikosi vya Israeli baada ya wanajeshi hao kuivamia kambi ya wakimbizi ya Jenin huko Ukingo wa Magharibi.

Mara kwa mara jeshi la Israeli kuzivamia nyumba za Wapalestina huko Ukingo wa Magharibi kwa lengo la kuwakamata wanaharakati na raia, mara nyingi huwashikilia bila kuwafungulia mashitaka.


Kwa mujibu wa makundi na mashirika ya haki za Wapalestina, Wapalestina kadhaa waliuawa na vikosi vya Israeli katika nusu ya kwanza ya mwaka 2013, huku wakiwateka Wapalestina wapatao 1,800, wakiwemo wanawake na watoto.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment