UTURUKI YAMKABIDHI IGP GARI KUCHUNGUZA WAHALIFU

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki Catalakaya (kulia) akikabidhi ufunguo wa gari la kuchunguza matukio ya uhalifu.



Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema amepokea gari moja aina ya VAN kutoka Serikali ya Uturuki kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa makosa ya jinai.

IGP Mwema alipokea gari hilo jana lenye mashine za kisasa kwa ajili ya kuchunguza matukio ya kihalifu yakiwemo makosa ya jinai, pamoja na ujambazi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mwema alisema ili kuwapata wahalifu yapo mambo ya kuzingatia ikiwa ni kukagua eneo la tukio, eneo lililofanyiwa uhalifu na mazingira ya tukio.

“Aidha alisema katika matukio ya kihalifu kunatakiwa kuwe na ushahidi wa kutosha unaovuka kiwango cha kuondoa mashaka katika uchunguzi,” alisema IGP.
Pia IGP Mwema alisema hadi kufikia sasa tunao askari 21 ambao wameweza kupitia mafunzo ya gari hiyo yenye vifaa vya kisasa kwa ajili yakupanua wigo wa kuweza kuwapata wahalifu.

Akizungumza katika mkutano huo, naibu katibu mkuu wa mambo ya ndani, Mwamini Malemi alisema gari hiyo yenye vifaa vya kisasa ni kwa ajili ya kupata uchunguzi mbalimbali baina ya majambazi.

Malemi alisema kifaa hicho kitasaidia jeshi la polisi kuondeza ujuzi katika suala la uchunguzi kwa kuwapata wahalifu, pia kumpata mhalifu wenyewe pasipo kuchukua picha ya mtu mwingine.


CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment