
Nchini Brazil, maafisa 25 wa polisi wamehukumuwa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa kuhusika na mauaji ya mwaka 1992 katika gereza la Carandiru yaliyogharimu maisha ya wafungwa 111.
Mapema leo Jumamosi, mahakama nchini humo iliwatia hatiani maafisa hao na kuwahumu kifungo cha miaka 624 gerezani kwa kutumia nguvu kupita kiasi katika kuamua ugomvi baina ya wafungwa.
Baada ya kesi iliyodumu kwa wiki nzima, jopo la mahakimu saba iliwatia hatiani maafisa hao kwa kuwaua wafungwa 52 katika kikao cha pili cha kesi hiyo yenye vikao vinne.
Ingawa waendesha mashitaka walisema kuwa wafungwa hao waliuawa, upande wa utetezi ulidai kuwa maafisa hao walikuwa wakijihami.
Manusura wanawatuhumu maafisa hao wa polisi kwa kuwafyatulia risasi wafungwa ambao walikuwa wameshajisalimisha au walikuwa ndani ya vyumba vyao.
Kila kikao cha mahakama kilijikita kwenye vifo vilivyotokea kwenye kila sakafu miongoni mwa sakafu nne za gereza la Carandiru katika mji wa Sao Paulo, mnamo Oktoba 2, 1992.
Kesi hiyo ililetwa mahakamani Aprili baada ya miaka 20 kupita tangu tukio hilo la kusikitisha lilipotokea.
Wakati wa kikao cha kwanza, maafisa 23 wa polisi walitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kutumika miaka 153 jela kwa vifo vya wafungwa 13.
Mwaka 2001, Kanali Ubiratan Guimaraes, mtu pekee ambaye alikuwa ameshitakiwa wakati huo, alihukumiwa kifungo cha miaka 632 jela.
Gereza la Carandiru likuwa na wafungwa wapatao 8,000 wakati tukio hilo likitokea na ndilo lililokuwa gereza kubwa kabisa katika eneo la Amerika ya Kusini wakati huo.
Gereza hilo lilibomolewa mwaka 2002.
0 comments:
Post a Comment