MAFURIKO YALETA MAAFA NCHINI SUDAN

A Sudanese man sits next to his house in a flooded street on the outskirts of the capital Khartoum on August 10, 2013.
Raia wa Sudan akiwa amekaa jirani na nyumba yake kwenye mtaa uliokumbwa na mafuriko katika viunga vya mji wa Khartoum, Agosti 10, 2013.



Mvua nzito iliyoandamana na mafuriko katika eneo la kaskazini la mji mkuu wa Sudan, Khartoum, imesababisha vifu vya watu 36.

“Watu thelathini na sita walifariki katika jimbo la Nile na nyumba 5,000 kuharibiwa vibaya kutokana na mvua na mafuriko makubwa,” Redio Omdurman iliripoti jana Jumapili.

Khartoum na eneo la jirani ziliathiriwa na mvua nzito siku ya Ijumaa, baada ya mafuriko yaliyoanza Agosti 1. Hata hivyo, ripoti hiyo haikutaja maafa hayo yalitokea kwa kipindi cha muda gani.

Mvua na radi siku ya Ijumaa viliendelea kwa muda wa saa nne katika mji Mkuu na kuharibu hata majengo ya kisasa.

Awali Umoja wa Mataifa ulikuwa umeripoti kwamba mvua na mafuriko katika mji wa Khartoum na maeneo mengine ya nchi hiyo yalisababisha vifo vya watu 11 na kuwaathiri wengine wapatao 100,000 katika mwezi wa Agosti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Umoja wa Umoja huo inayoratibu Misaada ya kibinaadamu (OCHA), vifo 9 katika 11 vilitokea Khartoum.

OCHA ilisema kuwa mbali na Khartoum na jimbo la Nile, mvua hiyo iliacha athari kubwa katika mikoa mingine mitano.

Aidha, ripoti hiyo iliashirikuwa zaidi ya nyumba 14,000 ziliharibiwa katika majimbo husika.

Lakini kabla ya mvua mpya, siku ya Ijumaa kundi la vijana linalojihushughulisha na misaada la Nafeer, lilitoa ripoti iliyoelezea kuwa idadi ni kubwa zaidi ya hiyo, na kusema kuwa kwa uchache nyumba 14,517 ziliharibika na zaidi ya watu  72,000 kuathiriwa katika wilaya nne za mji wa Khartoum.

“Baadhi ya familia bado zinaishi katika shule za jirani na ziko katika hali mbaya; maeneo mengi hayana umeme au usafiri,” lilisema kundi hilo.


Nafeer liliongeza kuwa familia katika maeneo haya hazikuwa na maji safi huku maji wanayotumia yanauzwa kwa mara mbili ya bei ya kawaida.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment