KILA BAADA YA DAKIKA 20 MWANAMKE MMOJA HUBAKWA NCHINI INDIA

Police try to stop supporters of India
Polisi wakijaribu kuwazuia wafuasi wa chama kikuu cha Upinzani nchini India cha Bharatiya Janata wakati wakiandamana kuelekea kwenye makazi ya mkuu wa chama tawala cha Congress nchini humo, Sonia Gandhi, wakati wa maandamano mjini New Delhi Aprili 21, 2013.



Maelfu ya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini India cha Bharatiya Janata (BJP) wamekuwa wakifanya mfululizo wa maandamano makubwa dhidi ya vitendo vya ubakaji vilivyofanywa na genge la wahuni katika jimbo lenye ufukara mkubwa la mashariki la Odisha.

Waandamanaji waliobeba bendera za chama cha BJP waliharibu magari na kutatiza usafiri wa reli mjini Bhubaneshwar, mji mkuu wa jimbo la Odisha.

Aidha, BJP kimeitisha mgomo mkubwa katika jimbo lote la Odisha kufuatia tukio la ubakaji lililofanywa na genge la wahuni na kifo cha binti mmoja mdogo. BJP kimeitaka serikali ya jimbo kuchukua hatua kali katika kushughulikia tukio hilo.


Tukio hilo linadaiwa kutokea Julai 28 ambapo binti wa miaka 14, ambaye alipigania uhai wake kwa siku 12, alifariki kutokana na majeraha akiwa hospitali baada ya kujichoma moto.

Tukio hilo ni tukio jipya kabisa katika matukio ya uhalifu wa kutisha yaliyowasha moto wa ghadhabu na maandamano nchini nzima.


Kwa mujibu wa Ofisi za Takwimu za Matukio ya uhalifu, mwanamke mmoja hubakwa ndani ya kila dakika 20 katika nchi hiyo ya pili kwa idadi kubwa ya watu duniani.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment