Jinamizi la mfululizo wa milipuko limeendelea kuundama maji mkuu wa Iraq, Baghdad, baada ya watu wapatao 70 kupoteza maisha na wengine 200 kujerihiwa vibaya sana.
Mamlaka za Iraq zinasema kuwa kiasi cha milipuko tisa kiliyatikisa maeneo yanayokaliwa na wafuasi wengi wa madhehebu ya Shia, wakati watu wakisherehekea maadhimisho ya sikukuu ya Eid al-Fitr.
Mlipuko mmoja ulitokea katika bustani moja katika mji wa Zubeidiyah, kusini mwa Baghdad, huku mingine ikitokea karibu na migahawa na maduka wakati wa saa za adhuhuri zenye harakati nyingi.
Mlipuko mwengine ulitokea jirani na soko katika kiunga kilichopo kusini mashariki mwa mji wa Baghdad, ambapo watu saba walipoteza maisha na 20 kujeruhiwa.
Katika tukio sawa na hilo, watu 10 walipoteza maisha yao na wengine 45 kujeruhiwa baada ya bomu lililotegwa kwenye gari kulipuka katika mtaa mmoja wenye shughuli nyingi katika mji wa Tuz Khurmato, kaskazini mwa Baghdad.
Milipuko hiyo, ambayo inaelezewa kupangiliwa vilivyo, ilikuwa sawa na ile iliyoutikisa mji wa Baghdad siku ya Jumanne, ambapo watu 50 walipoteza maisha yao.
Mashambulizi hayo mabaya yanakuja baada ya maafisa usalama wa Iraq kuweka hatua za ulinzi mkali nchini kote kwa ajili ya sikukuu za Eid.
Iraq imekumbwa na ghasia tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Kiasi cha watu 671 wameshauawa ndani ya mwezi wa Ramadhan pekee.
Terehe 1 Agosti, Umoja wa Mataifa ulisema kuwa jumla ya Wairaq 1,057 waliuawa na wengine 2,326 kujeruhiwa katika matukio ya ghasia mwezi wa Julai, na hivyo kuufanya mwezi huo kuwa mwezi mbaya zaidi tangu mwaka 2008.
Mpaka sasa zaidi ya watu 4,000 wamepoteza maisha katika mwaka huu wa 2013, huku mji wa Baghdad ukiwa mji uliokumbwa zaidi na mashambulizi hayo.
0 comments:
Post a Comment