POLISI KUWATAWANYA KWA NGUVU WAFUASI WA MURSI



Polisi wa nchini Misri wakishirikiana na vikosi vingine vya ulinzi na usalama wakiwa na zana nzito, wanatarajiwa kuchukua hatua kali dhidi ya wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani na jeshi, Muhammad Mursi, ambao wameweka makambi katika maeneo mbalimbali mjini Cairo.

Habari kutoka ndani ya vyombo vya kiusalama vya nchi hiyo, zimedokeza kuwa vikosi vyote vya usalama na ulinzi wa taifa vitatumika kuanzia leo katika mchakato endelevu ambao hatimaye utawaondosha kabisa waandamanaji mitaani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kikao kizito kilichofanyika baina ya waziri wa mambo ya ndani na washauri wake.

Ghasia na mivutano mikali ilishtadi nchini humo tangu Julai 3 baada ya jeshi kumuondosha madarakani Mursi. Vilevile jeshi lilichukua hatua ya kusimamisha matumizi ya katiba na kulivunja bunge.

Toke wakati huo, wafuasi wa Mursi wamekuwa wakifanya maandamano makubwa na kuweka kambi na mikusanyiko mikubwa wakitaka arejeshwe madarakani.

Mamia ya waandamanaji, wengi wao wakiwa wafuasi wa Mursi, wameuawa au kujeruhiwa katika ghasia zilizoitikisa nchi hiyo.

Mapema leo, Chama cha Muungano wa Kidemkrasia kinachopinga mapinduzi hayo, ambacho ni miongoni mwa vyama vikubwa kabisa nchini humo, kilisema kuwa kwa maandamano makubwa yamepangwa kufanyika katika maeneo mbalimbali ya mji wa Cairo kwa lengo la “kutetea uhalali” wa urais wa Mursi aliyechaguliwa kidemokrasia.

Mnamo Julai5, kiongozi mkuu wa chama cha Udugu wa Kiislamu, Muhammad Badie alisema kuwa kuondolewa kwa Mursi madarakani ni batili na mamilioni ya wafuasi wake wataendelea kufanya maandamano mpaka atakaporejeshwa madarakani. Aliapa “kuendeleza mapinduzi”  yaliyoudondosha utawala wa zamani wa rais Husni Mubarak mwaka 2011.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment