Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God, Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia leo katika hospitali ya Aman jijini Dar es Salaam.
Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.
HISTORIA FUPI YA ASKOFU MOSES KULOLA
Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.
Ni mume wa Elizabeth na wamezaa watoto10 ambapo saba bado hai.alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.
Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.
Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.
Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuna makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo
Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.
Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake.
Katika uhai wake, amepata kuwa na watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.

0 comments:
Post a Comment