·
Rais Robert Mugabe jana Ijumaa alitishia kuwapeleka jela mashoga na wasagaji watakaoshindwa kuzaa watoto wakati akizindua kampeni za chama chake kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Kiongozi huyo wa chama cha Zanu PF, ambaye ni mpizani mkubwa wa ndoa za jinsia moja, anasema kuwa alishtushwa kusikia kuwa Rais wa Marekani Barack Obama alizitaka nchi za Kiafrika kukumbatia ushoga.
Akisisitiza msimamo wake, Mugabe alitania kwa kusema: “Sasa (mashoga) watawezaje kuwa na watoto?
“Ninatamani niwafungie kwenye chumba nione kama watashika mimba; wasiposhika mimba basi wataenda jela kwa sababu wanadai kuwa wanaweza kuzaa watoto. Hivyo, tunasema: uchafu huo hapana, hapana, hapana!”
Akiendelea kuwapasua mbavu watu waliohudhuria kwa onyo lake hilo, Mugabe alienda mbali zaidi na kulikosoa Kanisa Angilikana kwa kubariki ndoa za mashoga ambazo alisema ni mwiko kwa Waafrika.
Aliwapa changamoto wasagaji wanaochukua nafasi ya wanaume katika uhusiano wao wathibitishe kama kweli wao ni ‘wanaume’.
“Wanawake nao wanajihusisha na uchafu huu. Sisi ni wanaume lakini ni kitu gani kinachokufanya udai kuwa wewe ni mwanaume?
“Tuonesheni uanaume wenu; mnataka kuwafanya wanawake wenzenu kuwa wake zenu na nyinyi kuwa waume zao? Sasa, huo ni wendawazimu; hatuwezi kuukubali,” alisema.

0 comments:
Post a Comment