MASHOGA WAIDUKUA TOVUTI YA SERIKALI YA NIGERIA




Wizara ya Habari ya Nigeria imethibitisha kuwa Alhamisi usiku tovuti ya taifa ilishambuliwa  kundi la wanaharakati wa haki za mashoga.

Katika taairifa iliyotolewa jana Ijumaa na Katibu wa Wizara ya Habari ya nchi hiyo, Bwana Joseph Mutah, shambulio hilo liligunduliwa na wizara yake na hatua za ziada zikawekwa ili kuzuia matukio kama hayo yanayoweza kujitokeza hapo baadaye.

Alisema, “Washambuliaji wanatoka kwenye kundi ambalo hivi karibuni lilizishambulia tovuti za serikali nyingi duniani, wakidai kuwa wanatetea haki za mashoga.

“Mashambulizi hayo ni uhalifu mkubwa unaofanywa ili kuzilaghai nchi zinazopinga mashinikizo yanayotolewa na mashoga kuhalalisha ndoa za jinsia moja kama zinavyofanywa katika baadhi ya nchi.

“Wakati tukitambua kuwa Nigeria ni nchi ya kidemokrasia na uhuru wa wananchi kutoa mawazo, ni kosa kwa yeyote ndani au nje ya nchi kutumia njia za kihalifu kuelezea au kutoa maoni yake. Wizara ya Habari itashirikisha mamlaka za uchunguzi kufanya uchunguzi wa shambulio lililotokea.

“Jamii ya Nigeria ni jamii iliyostaarabika na inayoheshimu misingi ya dini, ambayo watu wake wanaendelea kupinga kwa nguvu zote shinikizo lolote linalofanywa kuhalalisha ndoa za mashoga kama inavyofanyika katika baadhi ya nchi.
 “Wale wanaotaka kutulazimisha kuruhusu ushoga kutoka nje tunawashauri watumie njia halali na za kikatiba kutoa maoni yao kwa sababu serikali haitavumilia uhalifu wa kuvunja sheria zetu utakaofanywa na kundi lolote linalojificha nyuma ya kivuli cha kutetea haki za mashoga nchini.”



Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment