MAANDAMANO YALETA MAAFA MISRI

Supporters of the Egypt




Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kuwa kwa uchache watu watano  wamepoteza maisha na wengine 86 kujeruhiwa katika makabiliano yaliyotokea baina ya Rais aliyeuzuliwa Muhammad Mursi katika mji wa bandari wa Alexandria nchini Misri.



Vikosi vya usalama viliwavyatulia gesi ya kutoa machozi waandamanaji wanaomuunga mkono Mursi ili kuwatoa msikitini, huku watu kadhaa nje ya msikiti huo wakijeruhiwa kwa mawe wakati wa makabiliano baina ya pande mbili. Baadhi ya majeraha yalitokana na risasi za moto.


Aidha, maandamano wanaendelea katika maeneo mbalimbali ya mji wa Cairo ambapo wafuasi wa Mursi wamekusanyika katika mji wa Nasr na wale wanaoliunga mkono jeshi wakikusanyika katika Medani ya Tahrir. Kwa uchache watu 24 walijeruhiwa katika ghasia za Cairo.



Maandamano hayo yalifanyika katika kuitikia wito wa kufanyika kwa maandamano ya amani uliotolewa na chama cha Udugu wa Kiislamu kupinga mapinduzi ya hivi karibuni yaliyofanywa na jeshi kumuondoa Mursi. Katika taarifa yake ya jana Alhamisi, kiongozi wa chama hicho, Muhammad Badie, aliwataka Wamisri kumiminika mitaani kutaka urejeshwaji wa uhuru na demokrasia.

 

Wakati huo huo, mkuu wa jeshi la nchi hiyo, Jenerali Abdul-Fattah al-Sisi, alikuwa ametoa wito wa kufanyika maandamano makubwa nchi nzima yatakayolipa jeshi nguvu ya kupambana na kile alichokiita kuwa ni "fujo na ugaidi."


Muhammad Mursi ameendelea kuwa kizuizini katika eneo lisilojulikana baada ya jeshi kumuondoa madarakani kwa nguvu.


Watu kadhaa wameshapoteza maisha katika wimbi la ghasia zinazoendelea nchini humo baina ya wafuasi, wapinzani wa Mursi na vikosi vya usalama.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment