![]() |
| Waziri Mkuu wa Czech Petr Necas |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech Petr Necas ametangaza kujiuzulu kufuatia kashfa ya ufisadi na upelelezi inayomhusisha msaidizi wake.
“Kesho nitatangaza kujiuzulu kama waziri mkuu,” aliwaambia waandishi wa habari hapo jana, akaongeza kuwa, “Hivyo serikali yote itajiuzulu.”
Uamuzi wake wa kujiuzulu umekuja baada ya waendesha mashitaka kumfungulia mashitaka msaidizai wake Jana Nagyova kwa ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka Juni 14.
Uamuzi wake wa kujiuzulu umekuja baada ya waendesha mashitaka kumfungulia mashitaka msaidizai wake Jana Nagyova kwa ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka Juni 14.
Wabunge wawili wa zamani, waziri mmoja wa zamani na mkuu wa sasa na yule wa zamani wa upelelezi jeshini wametiwa nguvuni kuhusiana na kashfa hii.
Kwa mujibu wa Rais Milos Zeman, mashitaka hayo yaliyotolewa baada ya polisi kuzichunguza ofisi za serikali na ofisi binafsi za watu hao tarehe 12 Juni, ni mashitaka “mazito.”
Nagyova, ambaye amekuwa mtu wa karibu na waziri mkuu Necas kwa takriban muongo mmoja, anatuhumiwa kuwahonga wabunge hao wa zamani kwa kuwapatia nyadhifa katika makampuni ya serikali ili wao waviachie viti vyao vya ubunge.
Aidha, Nagyova anatuhumiwa kukiagiza kikosi cha upelelezi kuwachunguza, isivyo kisheria, watu kadhaa akiwemo mke wa Necas, Radka Necasova.
Hata hivyo, waziri mkuu amezitupilia mbali tuhuma hizo dhidi ya Nagyova na maafisa wengine watano, akisema “Mimi binafsi ninaamini kuwa sikufanya kitu chochote kibaya wenzangu wote pia hawakufanya jambo linalokwenda kinyume na uaminifu.”
Mapema, wapinzani wa Social Democrats walionya kuwa wangeendesha kampeni ya kutokuwa na imani na serikali ndani ya bunge mpaka bwana Necas ajiuzulu. Wakati huo huo, vyama vingine viwili vilivyo katika muungano wake wa mrengo wa kulia vilieza kuwa havikuwa tayari kumuunga mkono.
Vilevile, Necas alitangaza kuwa atajiuzulu katika nafasi yake ya mwenyekiti wa Chama chake cha mrengo wa kulia cha Civic Democrat Party.

0 comments:
Post a Comment