![]() |
| Mabasi yakiwa yamekwama katika barabara iliyokumbwa na mafuriko mjini Mumbai, India, Juni 16, 2013. |
Mvua za msimu zimesababisha mafuriko makubwa yaliyoua watu kadhaa katika jimbo lenye milima la kaskazini mwa India la Uttarakhand.
Mvua hizi za msimu vilevile zimesababisha hasara kubwa ya uharibifu wa nyumba, barabara, madaraja na mashamba.
Ripoti zinasema kuwa kwa uchache watu 13 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 50 hawajulikani walipo.
Tukio hilo limekuja baada ya mvua kubwa kuripotiwa katika maeneo mengi ya kaskazini na magharibi mwa India, huku majimbo ya Uttarakhand na Haryana yakiwa miongoni mwa maeneo yaliyoathirika vibaya.
Kwa uchache mahujaji 30,000 wa dini ya Kihindu wamekwama katika maeneo ya ibada na hija kwa dini hiyo katika Bonde la Kedarnath.
Helikopta za jeshi zimetumwa katika Jimbo la Haryana kwa lengo la kuwaokoa watu waliokwama katika vijiji vya ndani kabisa.
The monsoon season, lasting from June to October, cause floods with widespread destruction. This year, India’s monsoon rains are a month ahead of schedule.

0 comments:
Post a Comment